Uongozi wa Chadema Mkoa wa Rukwa, umesisitiza kuendelea na maandamano na mikutano 449, ili kupinga kile wanachokiita Utawala wa Kidikteta Tanzania (Ukuta).
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Rukwa, Shadrick Malila amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa kuhusu tamko lao kupinga Ukuta. Mweka Hazina wa Chadema Mkoa, Mary Mambwe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtowisa, amesema katika kufanikisha Operesheni Ukuta wamekusanya zaidi ya Sh20milioni kutoka kwa wadau mbalimbali, matarajio ni kufikisha Sh40 milioni.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amewatahadharisha Chadema kutofanya maandamano na mikutano hiyo Septemba Mosi kwani watakuwa wanakaidi maagizo na maelekezo ambayo Serikali imetoa.
No comments:
Post a Comment