Thursday, 18 August 2016

DC Kinondoni ataka Mganga Mfawidhi Mwananyamala asimamishwe.

Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza mkurugenzi wa manispaa hiyo kumsimamisha kazi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Delila Mushi kutokana na kuwapandishia wagonjwa bei ya kadi ya kumuona daktari . Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Ally Hapi alisema Kwa ufupi kuwa Hapo awali kadi hiyo ilikuwa ni Sh 3,000 ikapanda na kuwa Sh 6,000 lakini kuanzia Agosti Mosi mwaka huu ikapanda na kufika Sh 10,000, huku kadi hizo zikiwa bado zimeandikwa zinalipiwa Sh 3,000 ya awali.

No comments: