Maishahalisi.com

Tuesday, 16 August 2016

Tuesday,August,2016 Prof Ndalichako Abaini Wanafunzi Hewa Zaidi ya 1000 Vyuo Vikuu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesitisha malipo ya posho za kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini ambao wanafanya mafunzo kwa vitendo (practical training) ‘field’ baada ya kubaini kuwepo kwa wanafunzi hewa zaidi ya 1000 vyuoni. Prof. Ndalichako amesema wizara yake imezuia posho hizo kwa muda wa wiki mbili wakati wizara hiyo ikiwa inafanya uhakiki ili kuwabaini wanafunzi hewa zaidi pamoja na wahusika kuwachukulia hatua za kisheria. Aidha Prof. Ndalichako amewaagiza wakuu wote wa vyuo kuwasilisha taarifa za wanafunzi wao wizarani ili zoezi la kukagua na kubaini uahalali wa wanafunzi hao kuwepo vyuoni na wale watakaoonekana kuwa wana sifa watapatiwa posho zao za kujikimu mapema na kuendelea na masomo. CHANZO: EA RADIO.

No comments:

Post a Comment