Friday, 19 August 2016

Polisi Wanatumia Ubabe Kula Chips Bila Kulipa.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linafanya uchunguzi wa madai ya askari wake kula chipsi na kukataa kulipa kisha kuanzisha fujo baada ya kudaiwa fedha. Kwa ufupi Askari hao zaidi ya watatu wanadaiwa kuagiza watengenezewe chipsi mayai na kisha hukataa kulipa.

Kamanda wa polisi mkoani humo Muliro Jumanne amesema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 13 eneo la Mshikamano kata ya Ngokolo katika Mansipaa ya Shinyanga muda wa SAA NNE usiku.

No comments: