Mazoezi Hakuna asiyefahamu umuhimu wa kufanya mazoezi, lakini bado ni watu wachache sana wanaofanya mazoezi. Licha ya kuwa mazoezi yana faida kiafya cha ziada ni kwamba mazoezi, yanakufanya uwe mwerevu zaidi, mwenye furaha wakati mwingi, Husaidia kupata usingizi mzuri, na kukufanya ujisikie vizuri na mwili wako kwai hukuweka kwenye shepu nzuri.
2. Kutumia muda wako mwingi na marafiki na familia yako. Mahusiano ni muhimu sana kuliko unavyofikiria. Kujihisi huna mtu wa kuwa nae kama mwanafamilia ya rafiki kunaweza kukufanya ujisikie mpweke na idadi kubwa ya vifo vya watu wanaojiua huwa ni kwasababu ya upweke, na licha ya hilo unaweza ukapata magonjwa ya moyo, kisukari, n ahata kiharusi kwa sababu ya msongo wa mawazo. Watu wengi waliowahi kuishi kwa muda mrefu duniani wote ilithibika kwamba walikua na mausiano mazuri na walijihusisha sana na jamii. Ukiwa na ujumbe mzuri, shirikiana na wenzio, na wenzio wakiwa na ujumbe mzuri furahia.
3. Kuwa na shukurani. Unaambiwa shukuru Mungu wako kwa kila jambo, sio tu kwasababu una Imani nae, iwe pia kwasababu yako mwenyewe, hapo utakuwa mwenye furaha, utajisikia vizuri na itakujengea mahusiano mazuri na watu wako wa karibu. Yaani kifupi itakusadia kuwa kuishi vizuri na
watu na maisha utayaona marahisi.
4. Kupata usingizi wa kutosha. Huwezi kujinyima kulala na ukadhani haitakuathiri, uchovu utakaoupata itakufanya iwe ngumu kwako kuwa na furaha na la ziada Kukosa usingizi itakusababishia ugonjwa. Pumzisha mwili wako ili uweze kuwa fit siku inayofuata. Mwili wako ni kama mashine nyingine yeyote, unataka kupumzika vya kutosha.
5. Kucheka/Kufurahi Watu wanaotumia ucheshi kukabiliana na msongo wa mawazo, huwa na mifumo ya kinga madhubuti, hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kisukari. Cheka kila siku kwa kujikumbusha vitu au mtu anayekufa ufurahi, utajisikia vizuri wewe na uhusiano wako na uliyemkumbuka utazidi kushamiri.
6. Kugusana na mtu. Kumgusa mtu husadia kupunguza stress, uwezo wako wa kufanya kazi na mtu unaongezeka, husadia pia kuwa mshawishi. Mfano mzuri ni kumbato, kumkumbatia mtu, au mtu kukukumbatia huongeza furaha. Vile vile kujamiiana huzuia mtu kupata ugonjwa wa moyo, na saratani na kufanya mfumo wa kinga huiimarika zaidi na pia kujamiiana huongeza siku za kuishi.
No comments:
Post a Comment