Thursday, 22 September 2016

Jamaa Afumwa Akimbaka Mbuzi.

Hekaheka ya September 21, 2016 ilitokea Moshi Mkoa wa Kilimanjaro ambapo kuna stori hii ya mbuzi aliyebakwa kwa masharti ya mganga. Tukio hilo limefanywa na kijana ambaye anadai alikwenda kwa mganga wa kienyeji ili kupata dawa za kuwa tajiri ndipo akapewa masharti ya kufanya tendo la ndoa na dada yake wa kuzaliwa au afanye tendo hilo na mnyama. Akielezea tukio hilo Mlinzi wa eneo alipobakwa Mbuzi huyo anasema "Jana jumapili alikuja saa nane za usiku akanikuta nimekaa kwenye viti hivi akaniuliza umelala? nikamwambia eh nimelala asijue kama namtega akazunguka na kuingia kwenye zizi la mbuzi na mbuzi wakawa wanakimbia, nikazunguka kwenda kwenye zizi nikasikia mbuzi analia’ ‘Nikamuona ameinama karibu na mbuzi nikamulika tochi na kumuuliza Sangao unafanya nini akashtuka na kulalia tumbo kisha akaanza kuomba msamaha, nikamwambia ukikimbia nakupiga mkuki na ukiruka fensi nakupiga mishale" anasema Mlinzi.

Baada ya kukamatwa na kubanwa jamaa huyo alijitetea kwamba alitumwa na mganga aende akafanye mapenzi na dada yake wa kuzaliwa hivyo alishindwa kufanya hivyo ndipo mganga akamwambia atafute mnyama akafanya naye tendo hilo.

No comments: