
04/09/2015
Mwanza
By SirLalian Mwittah Nyalali.
Mwenyenacho ni dhahabu
Kila mtu husikiliza
Yake sauti
Sababu alivyo
Hii ni dunia yetu.
Hii ni dunia yetu
Alivyo imetawala
Ujuzi mwingi ninao
Basi sifahamiki
Nani atwishwe mzigo?
Mwanadamu ndani ya mfumo.
Akiwa nje ana sauti
Aingiapo ndani hufunga mlango
Husahau walio nje
Sababu haonekani
Nje kuna makundi
Yakiwa mlangoni
Aliye ndani afungue mlango.

© 2016 haki zote zimehifadhiwa.
No comments:
Post a Comment