Saturday, 1 October 2016

Marekani Yapigilia Msumari Tatizo La Ajira Tanzania.


MAREKANI yapigilia msumari tatizo la ajira Tanzania, yaisaidia Tanzania walimu 51 wa Sayansi na Hisabati.

Mark Childress, Balozi wa Marekani nchini Tanzania.
Katika hafla ya kuwaapisha walimu hao jijini Dar es Salaam, Kaimu Balozi wa Marekani Virginia Blesa amesema walimu hao watakaofanya kazi katika mikoa 22 watasaidia kupunguza tatizo la walimu wa masomo ya Sayansi nchini.

Bleisa amesema kuwa wapo walimu wengi wanatamani kufundisha kwa kujitlea nchini katika nyanja mbalimbali kupitia mpango wa kusaidia elimu ulioandaliwa na marekani kwa nchi masikini duniani.
Kwa upande wao walimu hao wamesema kuwa wanategemea wanafunzi watanufaika na elimu watakayowapa na kuomba ushirikiano kwa walimu watakaowakuta katika shule walizopangiwa.

Chanzo: EATV




© 2016 all rights reserved

No comments: