KIDUME UKIZIONA DALILI HIZI 4 UJUE BASI ANAKUPENDA SANA NA YUKO TAYARI KUFANYA JAMBO LOLOTE KWA AJILI YAKO.
UTAJUAJE KUWA MWANAMKE ANAKUPENDA KWELI
Ni muhimu sana kwako mwanaume kujua kwa uhakika kuwa mwanamke anakupenda kweli kweli,utajuaje kuwa mwanamke anakupenda? Zifuatazo ni ishara ambazo wewe kama mwanaume unapaswa kuwa makini ili uweze kuziona na kuzifanyia kazi;
1#Mwanamke anayekupenda. Atakuwa tayari kujitoa muhanga kwa ajiri yako yaani kujitoa kafara mfano, vipo vitu ambavyo watu wengine hawawezi kuvifanya ila isipokuwa kwa wale wanaowapenda kwa moyo wote. Je wewe ni sehemu mojawapo ya vitu vichache anavyovipa kipaumbele? Je wewe unakuwa wa kwanza mbele ya rafiki zake? Je anakufanyia vitu ambavyo hawezi kuwafanyia wanaume wengne?Je ameacha mambo mengine ili aweze kuwa na wewe? Ni kwa vitu kama hivi unaweza kutambua wewe ni wa muhimu kwake.
2# Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako,mtu anayekupenda atahangaika juu ya usalama wako,raha yako,heshima yako na maendeleo yako.Hii ni moja kati ya ishara kubwa kuwa mwanamke uliyemlenga anakupenda kweli.
3# Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa,ingawaje wivu mara nyngne unaweza kuvuruga penzi endapo utazidi.Wivu ni ishara kuwa anakupenda wewe na anataka akulinde usiibiwe au asije akakupoteza,anaogopa usije ukatoka katika maisha yake,au kwa maneno mengine usije ukamtoa moyoni mwako na nafasi yake ikachukuliwa.
4# Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu wengine atacheka nao lakini atakugeuzia wewe macho namaanisha uso wake haraka sana. Kufanya hivi ni kuonyesha kuwa anakuhesabia wewe kuwa utaweza kumletea furaha katika maisha yake,zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa utamuona kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu wa furaha. Asante sana kwa kutembelea blog hii pia endelea kufanya hivyo kila Siku ili upate habari moto moto.
Wako mwandishi~~~~~Sir Lalian Nyalali Mwittah.
No comments:
Post a Comment