#Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji na Mafuta (EWURA), imetangaza kushuka bei ya mafuta ya aina zote kwa jumla na rejareja.
Bei hizo mpya hazitahusisha mkoa wa Tanga .
#Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi, alisema katika katika taarifa yake kuwa, bei hizo za mafuta zimeshuka kwa viwango tofauti tofauti. Petroli imeshuka kwa Sh 65, Dizeli Sh 63 na Mafuta ya taa Sh 86. Bei ya jumla imepungua ambako kwa petroli ni Sh 65.31, dizeli Sh 63.39 na mafuta ya taa Sh 85.93. Akieleza sababu za kushuka kawa gharama hizo, Mkurugenzi Mkuu alisema kuwa kushuka kwa bei ya petroli katika soko la dunia na kupungua kwa gharama za usafarishaji/uletaji wa mafuta hayo nchini, ndizo sababu kuu zilizochangia kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la ndani nchini. “Bei ya jumla na rejareja kwa petroli na dizeli katika Mkoa wa Tanga imeongezeka kidogo ikilinganishwa na toleo la bei za mafuta hayo lililopita la Agosti 3, 2016.
#Kwa upande wa mkoa wa Tanga, bei ya rejareja kwa petroli na dizeli imeongezeka kwa viwango ambavyo petroli ni Sh 50 na dizeli Sh 19. Kwa kulinganisha na matoleo haya mawili, bei ya jumla imeongezeka. Petroli Sh 49.61 kwa lita sawa na asilimia 2.80 na dizeli Sh 18.57 kwa lita sawa na asilimia 1.1. “Ongezeko hili la bei limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kupokea mafuta mapya (petroli na dizeli) ndani ya Agosti 2016, ambayo yalitarajiwa kupokewa Julai 2016 na pia kutokupokea mafuta mapya kutoka katika meli ya MT. Nevaska Lady ndani ya Agosti mwaka huu,” alisema Ngamlagosi. Hata hivyo, alisema mamlaka hiyo inawakumbusha wananchi kwamba bei kikomo ya mafuta kwa eneo husika, pia inapatikana kupitia simu zao za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kufuata maelekezo.
No comments:
Post a Comment